Makubaliano ya Ushirikiano kati ya RAC na St. Partick Sch

Utiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati ya chuo cha Regional Aviation College na Shule ya St. Patrick Arusha katika kufundisha masomo ya usafiri wa anga.


Source: Q Media

July, 2024

Mkurugenzi mtendaji wa Chuo cha usafiriwa wa anga cha Regional Aviation ameeleza kuwa kukosekana kwa elimu ya masuala ya anga kwa watanzania, imepelekea wanafunzi kushindwa kufanya uchaguzi katika masomo ya usafiri wa anga, hali inayopelekea kukosekana kwa wataalamu wa kutosha katika sekta hiyo na kusababisha fursa nyingi katika sekta ya anga kuchukuliwa na watu kutoka mataifa mengine.

Hali hii imepelekea msukumo wa ushirikiano kati ya Chuo cha Regional Aviation na Shule ya St. Partick Arusha ili kuweza kuwafundisha wanafunzi wa Sekondari masomo ya usafiri wa anga, aidha ushirikiano huu utasaidia kuwasaidia wanafunzi kupata uelewa mpana juu ya sekta ya anga na kutambua uwepo za fani nyingi zaidi ya Urubani, ikiwemo fani za mafundi wa ndege, wahudumu wa ndani ya ndege, wahudumu katika viwanja vya ndege, waongoza ndege na fani nyingine nyingi katika sekta ya anga.

Chuo cha Regional Avation kinatoa kozi mbalimbali za usafiri wa anga ikiwemo,  Air Cargo Operations, Airport Operations, Cabin Crew, Air fares and Ticketing, Flight Dispatch/Operations na Passengers and Aircraft Handling, hii ikiwa ni fursa na uwanja mpana kwa wanafunzi wanaomaliza masomo yao ya sekondari kujiunga na kozi hizi ili kunufaika na fursa zilizopo katika sekta ya usafiri wa anga.


Makubaliano haya kati ya Chuo cha Regional na Shule ya St. Patrick Arusha sio tu yatainufaisha sekta ya usafiri wa anga bali hata sekta ya utalii nchini ambayo kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sekta hii yanategemeana na uimara na ukuaji wa sekta ya anga.

Aikongea katika Mahojiano yetu Bi. Victoria amewasihi wazazi na walezi kuwapa uhuru watoto wao ili kuweza kufanya machaguo wayapendayo ikiwa ni pamoja na taaluma katika masuala ya usafiri wa anga, sekta ambayo ajira zake zipo wazi na zinapatikana kwa



Fursa za ajira

Makubaliano haya yatawasaidia wanafunzi na wahitimu wengi kingia katika sekta yenye wigo mpana na fursa nyingi za ajira.

Ukuzaji wa Sekta ya Anga

Makubaliano haya yatasaidia ukuaji wa sekta ya anga Tanzania.

Ukuzaji wa Sekta ya Utalii

Ukuaji wa sekta ya anga ni kichocheo cha ukuaji wa sekta ya utalii Tanzania.

Related Posts

 

Comments

No comments made yet. Be the first to submit a comment
Already Registered? Login Here
Guest
Wednesday, 22 January 2025

By accepting you will be accessing a service provided by a third-party external to https://aviationcollegetanzania.com/

Aviation Courses

Join us for the best Aviation Courses

Business Courses

Join us for the best Business Courses

Teaching Facilities

We go beyond your academic needs